Sunday, January 31, 2016

Wahitimu vyuo vikuu kupatiwa ujuzi .


Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo ya fani wanazosomea na badala yake watumie fursa zilizopo kujiongezea ujuzi wa kufanya kazi.
Rai hiyo imetolewa kufuatia wasomi wengi kudaiwa kushindwa kuajiriwa kwa kukosa ujuzi wa fani walizosomea.
 Ni katika mkutano wa wajasiriamali na wakufunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ,  ambapo Prof Ganka Nyamsoro, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Tawi la Dar Es Salaam amesema,  chuo hicho kimechaguliwa kusimamia mradi wa kuwasaidia wahitimu kupata nafasi katika kampuni  za wajasiriamali ili waweze kujiongezea uzoefu  na kupata ajira.
Mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la SWEDENI umelenga kutoa fursa kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu kupata uzoefu wa yale waliyosomea chuoni.
 Kwa upande wa Wajasiriamali hao  wadogo na kati wamesema kwao ni Fursa Muhimu Kwakuwa watafanya kazi na watu wenye Taaluma,Huku wahitimu nao wakipata  ujuzi kutoka kwao.
Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la ajira mbali na kuwa Serikali imejitahidi kuwekeza katika elimu.

No comments:

Post a Comment