Sunday, January 31, 2016

Mkuu wa Shule ya Sekondari Komakya avuliwa madaraka.



kili

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Novatus Makunga amelazimika kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komakya iliyoko Mkoani Kilimanjaro kufuatia kukiuka maagizo ya Mkuu wa Mkoa ya kuwa vikao vyote vinavyohusiana na michango ya wanafunzi kati ya wazazi na uongozi  wa shule kutolewa ufafanuzi kabla michango hiyo haijaanza kukusanywa
Hatua hiyo imekuja kufuatia simtofahamu iliyojitokeza kati ya wazazi wa wanafunzi na uongozi wa shule uliotolewa ya kwamba kabla ya michango kukusanywa ni lazima Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupewa Taarifa.
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Komakya iko umbali wa km 18 kutoka moshi mjini amelalama kuhusu kupoteza muda mwingi akifuatilia ada.
Sintofahamu ilijitokeza   kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo mara baada tu walimu wa shule iyo kuwarudisha ada wanafunzi huku wakitaka kupewa ufafanuzi kuhusiana tamko la mh. Rais kuhusu elimu bure
Kufuatia suala hilo Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini Novatus Makunga akalazimika kufika shuleni hapo na baada ya kusikiliza pande zote kumvua madaraka Mkuu wa Shule hiyo Bi.Rose Ngoti kufuatia kufanya maamuzi na wazazi wa shule kwa kuchangisha michango pasipo kuishirikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama waraka wa seriklai unavyozitaka shule hizo
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mjini ina jumla ya shule za Kata 57 wanafunzi 25,402 walimu 1300 huku changamoto kubwa ikiwa ni upungufu wa walimu wa sayansi katika shule hizo.

Zoezi la kutoa kivuko kilichozama lakutana na wakati mgumu

kivuko

Licha ya kuwasili kwa mitambo  kusaidia zoezi la uokoaji wa kivuko kilichozama, zoezi hilo limeshindwa kufanyika kwa ufanisi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha toka saa saba usiku hadi majira ya saa kumi jioni kukwamisha zoezi hilo pamoja na juhudi za kuvuta kivuko hicho kushindikana.
Hata hivyo huduma ya mawasilinao baina ya upande wa Ulanga na Kilombero imeweza kurejea mara baada ya Wizara ya mawasilinao ujenzi na uchukuzi kufanikiwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu ili waendelee na safari.
Zoezi la uokoaji na uvutaji wa kivuko  ch MV Kilombero limezidi kuwa gumu, kutokana na changamoto ya vifaa vya uokozi, pamoja na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo  hilo, hivyo kukwamisha juhudi zinazoendelea kutolewa na mamlaka za uokozi.
Licha ya kutumia helkopta ya jeshi la Polisi kutafuta kama kuna watu ambao walisombwa na maji, juhudi hizo zimegonga mwamba baada ya kutopatikana kwa mtu hata mmoja.
 Hata hivyo juhudi zilizofanywa na wizara ya uchukuzi kwa kushirikiana na vikosi vya uokoaji kutoka kikosi cha wanamaji, vimefanikiwa kurudisha mawasiliano ya pande hizo mbili, kwa kuanza kuvusha wananchi wa kilombero na ulanga kwa kutumia boti za mwendo kasi. .
Wananchi wameiomba serikali kuongeza jitihada katika zoezi la uokoaji, na kuishukuru kwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu.
Zoezi la kukitoa kivuko na kukivuta nchi kavu  limeshindikana kwa siku ya jana kutokana  na kunyesha kwa mvua hiyo pamoja na mitambo iliyopelekwa kuvuta, kushindwa kufanikiwa.

Wahitimu vyuo vikuu kupatiwa ujuzi .


Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo ya fani wanazosomea na badala yake watumie fursa zilizopo kujiongezea ujuzi wa kufanya kazi.
Rai hiyo imetolewa kufuatia wasomi wengi kudaiwa kushindwa kuajiriwa kwa kukosa ujuzi wa fani walizosomea.
 Ni katika mkutano wa wajasiriamali na wakufunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ,  ambapo Prof Ganka Nyamsoro, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Tawi la Dar Es Salaam amesema,  chuo hicho kimechaguliwa kusimamia mradi wa kuwasaidia wahitimu kupata nafasi katika kampuni  za wajasiriamali ili waweze kujiongezea uzoefu  na kupata ajira.
Mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la SWEDENI umelenga kutoa fursa kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu kupata uzoefu wa yale waliyosomea chuoni.
 Kwa upande wa Wajasiriamali hao  wadogo na kati wamesema kwao ni Fursa Muhimu Kwakuwa watafanya kazi na watu wenye Taaluma,Huku wahitimu nao wakipata  ujuzi kutoka kwao.
Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la ajira mbali na kuwa Serikali imejitahidi kuwekeza katika elimu.

Hii Ndio Sababu ya Rais Magufuli Kumuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange..

RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .

Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Friday, January 29, 2016

TUNDUMA AND NAKONDE ENVIRONMENT.

UJASILIAMALI NA BIASHARA .

     
  Pata mambo matamu ili kama ni mwajiriwa au umeajiliwa soma HAPA MAUJANJA UJASIRIAMALI NA BIASHARA KIUJUMLA.
Nimekuwa nikishauri watu wanaoingia kwenye biashara na ujasiriamali kwa muda sasa lakini sijawahi kumwambia mtu aache kazi haraka ili aweze kuweka nguvu zake kwenye ujasiriamali. Nina sababu nyingi kwa nini sifanyi hivyo, na hapa nitakushirikisha sababu kumi.

1. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato cha uhakika. Japokuwa kazi haina uhakika sana kwa sasa, lakini angalau kwa sasa kuna kipato ambacho unakipata kwenye ajira yako. Hiki kitakuvusha nyakazi ambazo ni ngumu, hasa pale ambapo utaanza ujasiriamali ukiwa bado kwenye ajira yako.

2. Kuna nafasi nyingi za kuweza kuanza ujasiriamali hata bado ukiwa kwenye ajira yako. Tumia nafasi hizi na anza kidogo kidogo, jifunze kwenye kila hatua unayoshindwa au kukosea, endelea kukuza biashara yako na ikifikia hatua ukaona sasa hapa inaweza kukupatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yako ndio unaweza kuacha kazi.

3. Kutoa fedha kwenye biashara changa ni kuiua. Katika miezi angalau sita ya kwanza ya biashara yoyote ndio kipindi ambacho biashara yoyote inakazana kukua. Sasa kama utaondoa fedha kwenye biashara hii kwa sababu yoyote ile, unakuwa umeandika adhabu ya kifo kwneye biashara yako. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato kingine unachotegemea tofauti na biashara hiyo, hivyo kama umeajiriwa, hiki ndio kipato chenyewe.

4. Kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unapokuwa kwneye kazi ni rahisi sana kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unaweza kutengeneza wateja wengi wa huduma au bidhaa zako kupitia kazi unayofanya hivyo inakupa nafasi nzuri ya kuweza kukuza biashara yako.

5. Kufaidi huduma nyingine muhimu. Kuna huduma muhimu ambazo utaweza kuzifaidi kama utakuwa kwenye kazi. Kupitia kazi yako unaweza kuwa unapata huduma ya bima ya afya kwako na kwa familia yako. Hii inakusaidia kuokoa fedha nyingi ambazo ungezitumia kwenye huduma za afya. Japokuwa unaweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya kama mtu binafsi, bado itakugharimu kiasi kikubwa kuliko aliyeko kwneye ajira.

6. Kazi inaweza kukupa uzoefu wa biashara. Kuna baadhi ya biashara unazoweza kuanzisha ambazo zinaendana na kazi unayofanya sasa. Kwa kuwepo ndani ya kazi ile unajifunza mambo yote muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kukuza biashara yako. Pia unawajua vizuri wateja ambao wanaweza kuja kuwa wateja wako pia na mambo mengine ya ndani ambayo yatakuwezesha kuendesha biashara yako vizuri.

MAMBO YA BOARDER KILA MTU YU BUZZ

http://lusakavoice.com/wp-content/uploads/2014/05/Nakonde-border.jpg

Kambi Rasmi Ya Upinzani Yagoma Kusoma Hotuba Yao Bunge Lasitishwa .

Bunge
Kwa mara nyingine bunge limesitisha shughuli zake baada ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kugoma kusoma hotuba yao ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

Hali hiyo imejitokeza baada ya Mh Zitto kuomba mwongozo na kusema "Serekali imefanya makosa kwa kuwasilisha mpango huo kwa mwaka mmoja mmoja jambo ambalo ni kinyume na kanuni na katiba yetu
Wakati Zitto anaomba mwongozo, alimwomba mwenyekiti wasitishe shughuli mpaka marekebisho yakafanyike. Lakini Chenge alikataa, Cha kushangaza baada ya upinzani kugoma kuwasilisha Hotuba yao ghafla alisitisha.

Nimejiulizaa alichomkatalia Zitto ni nini na alichokuja kukifanya ni nini?

Monday, January 25, 2016

ACT washtukia ruzuku ndogo mpango wa elimu bure.


Umoja wa Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo wa Jijini Dar es Salaam umesema umeshtushwa na kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa na serikali kwa ajili ya kutekelza mpango wa elimu bure.


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe
Katika taarifa yao waliyoitoa kwa vyombo vya habari jana Jijini Dar es salaam umoja huo umesema kuwa kiasi hicho cha fedha kilichotengwa ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji muhimu ya upatikanaji wa elimu bora nchini.
Ngome hiyo ya Vijana wa ACT Wameitaka serikali iongeze kiasi cha ruzuku ili kukidhi dhana ya elimu bure na mahitaji ya shule hadi kufikia sh.elfu 40 kwa kila mwanafunzi wa sekondari na sh. elfu 25 kwa mwaka kwa mwanafunzi wa shule ya msingi.
Aidha katika taarifa yao hiyo vijana hao wameziomba kamati za shule za wazazi kufuatilia kwa karibu fedha hizo za ruzuku na matumizi yake kwa shule husika ili kuepuka ubadhilifu wa aina yoyote.

Friday, January 22, 2016

Rais Magufuli Asema Hataki Kusikia Malalamiko ya Wananchi juu ya Suala la Njaa......Ikitokea Akasikia, Mkuu wa Mkoa Atafukuzwa Kazi .


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amesema kuanzaia sasa hataki kusikia malalamiko ya wananchi juu ya suala la njaa na ikitokea akasikia vilio hivyo vikiendelea mkuu wa mkoa husika atachukuliwa hatua ikiwemo ya kufukuzwa kazi.
 
Mh. Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ameyasema hayo alipokuwa njiani kutoka jijini Arusha kwenda wilaya Monduli kwa ajili ya kufunga mazoezi ya kijeshi ya kuonyesha uwezo wa medani 2016 yaliyofanyika katika Briged ya 303 iliyoko Monduli.

Aidha Mh rais Dr. Magufuli amesema ni jambo halikubali kuendelea kusikia malalamiko ya wananchi juu ya mambo yaliyoko ndani ya uwezo na yanayoweza kutatuliwa na wakuu wa mikoa na ameendelea kuwataka viongozi na watendaji wa serikaali kutimiza wajibu ukiwemo wa kuwatumikia wananchi.

Kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya kero ya rushwa mh Rais amewataka wananchi hao kuwa wapole kwani kero itashughulikiwa na itapata ufumbuzi kwani zoezi la kutumbua majipu linaendelea na kwamba kinachofanyika sasa ni  kutumbua majipu yaliyoiva ambayo ni sehemu ndogo tu ya majipu yaliyopo.

Mh Rais kesho anatarajiwa kutoa kamisheni kwa askari wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha TMA monduli.

Thursday, January 21, 2016

MATOKEO HAPA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.

Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.

Wednesday, January 20, 2016

HISTORIA YETU

Historia
Asili ya jina Mbeya ni neno la Kisafwa ‘Ibheya’ likimaanisha chumvi. Wafanyabiashara wengi walifika eneo hilo kubadilisha chumvi na mazao yao. Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mwaka 1927 kufuatia kushamiri kwa upatikanaji wa dhahabu kwenye milima ya Loleza na mkondo wake kufika Chunya eneo la Lupa Tingatinga. Hata leo eneo la kati la jiji la Mbeya huitwa Lupa Way kama ilivyozoeleka miaka hiyo ambapo mahema ya wafanyabiashara wa Kihindi yaliwekwa wakiwa njiani kwenda Lupa.
Jografia ya mji wa Mbeya na historia ya makanisa makongwe iliathiriwa na ubaguzi uliowekwa na wakoloni Waingereza.
Eneo la Uzunguni lilitengwa kwa ajili ya Waingereza waliokuwa watawala. Hata makao makuu ya serikali ya Jimbo yalikuwa eneo hilo. Hivyo kanisa la Waingereza, Anglikana limejengwa mwanzo wa Uzunguni karibu kabisa na makao makuu ya mkoa na wilaya ya Mbeya.
Eneo la Uhindini, Lupa Way litengwa kwa ajili ya Wahindi kutoa Goa walikuwa wakifanya biashara hapo. Kwa kuwa kanisa la Katoliki lilikuwa likihudumia Wahindi hao na wazungu wachache Waeire (Irish) lilijengwa katikati la eneo la Uzunguni na Uhindini.
Eneo la Majengo litengwa kwa ajili ya Waafrika. Kanisa la Moravian ambalo ndilo dhehebu la Kikristo asilia la Mbeya, lilijengwa Majengo karibu na Sokomatola ambako Waafrika waliishi. Miongoni mwa Waingereza hapakuwepo na Mmoravian hata mmoja.
Mji wa Mbeya uliendelea kupanuka pande zote isipokuwa eneo la Kaskazini lilitawaliwa na milima. Ujio wa Wanyakyusa kutoka Rungwe ndiyo ulioleta Uluteri mjini Mbeya.
Wakazi
Wasafwa ambao ndiyo wenyeji halisi wa mji wa Mbeya wamekuwa wakihamia milimani kupisha wageni. Kukua kwa kasi kwa jiji la Mbeya kumepelekea wenyeji hao kuuza maeneo yao na wao kurudi maeneo ya milimani wakiendelea na kilimo na ufugaji kidogo. Leo hii eneo la wilaya ya Mbeya ambako ndipo jiji lilipo limetawaliwa zaidi na Wanyakyusa na Wakinga wakiwa ndiyo wafanyabiashara wakubwa na Wahindi pia.
Wenyeji wengine wa wilaya ya Mbeya ni Wamalila.
Wenyeji wa wilaya za Rungwe na Kyela ni Wanyakyusa. Wenyeji wa wilaya ya Ileje ni Wandali. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu ingawa watu waishio huko zaidi ni Wanyiha. Wenyeji wa wilaya ya Mbozi ni Wanyiha na Wanyamwanga, lakini mji wa Tunduma umetawaliwa zaidi na Wakinga ambao ndiyo wafanyabiashara wenye kumiliki uchumu wa mji huo mdogo. Wenyeji wa wilaya ya Mbarali ni Wasangu, Wawanji, Wabena na Wakinga.
HII NI MBEYA WANAKOPATIKANA WANYAKYUSA

2015 mwaka wa historia mji wa tunduma.

AIRTEL MKWANJIKA YATUA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, WASHINDI NANE WAJIZOLEA FEDHA.

Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akipewa maelezo kabla ya kuingia kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde


Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akiwa kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde akiendelea kujikusanyia mapesa.

Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akishuhudia fedha alizookota zikihesabiwa katika shindano la kwangua ushinde

Iddi Yusufu akiendelea kuokota fedha katika boksi kwenye shindano la kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika

Mshindi  Jotham Mwainyekule akijaribu bahati yake kama anaweza kuokota fedha zote ambazo ni shilingi Milioni Moja anazopaswa kuziokota kwa muda wa sekunde 60

Menena Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini, Straton Mushi akielezea namna zoezi la Kwangue ushinde linavyofanyika na washindi wanavyopatikana ambapo kwa Kanda jumla ya washindi nane wamepatikana



Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia shindano la Kwangua ushinde la Airtel Mkwanjika

Mshereshaji wa Airtel Mkwanjika akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa shindano kwa washindi kuokota fedha

Mmoja wa Watumishi wa Airtel akionesha mfano jinsi ya kushiriki zoezi la kuokota fedha linavyopaswa kufanyika

PROMOSHENI inayoendeshwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel inayojulikana kwa jina la Kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika imetua katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini ambapo washindi nane wamepatikana na kujizolea fedha taslimu.
Zoezi la kuwapatia zawadi washindi hao lilifanyika jana katika ofisi za Kanda za Airtel zilizopo Uhindini Jijini Mbeya na kushuhudiwa na wakazi wa Jiji hilo kutokana na zoezi hilo kufanyika katika maeneo ya wazi.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini, Straton Mushi alisema tangu shindano hilo lianze mwezi Disemba mwaka jana nchi nzima wateja wengi wamejitokeza na kujizolea fedha lukuki ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika kuboresha hali yao ya kiuchumi kwa kuongeza vipato vyao.
Alisema hakuna masharti yoyote ya mteja kujishindia bali anachopaswa ni kununua vocha na kuikwangua kasha kuijaza kwenye simu yake ya Airtel anakuwa ameingia moja kwa moja kwenye shindano ambapo baada ya kuchaguliwa huingizwa kwenye boksi maalum lenye fedha taslimu shilingi Milioni moja ambazo hupulizwa na upepo hivyo kasi ya mteja kuokota fedha ndizo zinakuwa zawadi yake.
Aliwataja washindi walioshiriki kujiokoteza fedha kwa Kanda kuwa ni pamoja na Ismail Mwaswale (Sumbawanga) ambaye kwenye boksi alijiokotea jumla ya shilingi 920,000 kwa muda wa sekunde sitini akifuatiwa na Iddi Yusufu (Iringa) aliyeokota shilingi 750,000 na Jotham Mwainyekule mkazi wa Mbozi aliyepata shilingi 730,000/=.
Aliwataja washindi wengine kuwa ni Kazembe Salamanda Mkazi wa Ruvuma, Onesmo Lubaga mkazi wa Iringa, Tonny Moris Mkazi wa Mbeya, Bahati Muhawala mkazi wa Mbeya na Thomas Baraka mkazi wa Rukwa ambao viwango vyao havikujulikana mara moja.
Wakizungumza baada ya kumalisha shindano hilo washindi hao walitoa wito kwa watanzania kuiamini Airtel na kuitumia kwa kuwa huduma zao ni za kweli na uhakika tofauti na madai ya wengi kuwa promosheni hizo ni danganya toto.
Ismaila Mwaswale(43)Mkazi wa Sumbawanga na mfanyabiashara mdogo alisema baada ya kupigiwa simu kwamba ameshinda hakuamini hadi pale alipotumiwa nauli ya kuja kushiriki zoezi hilo mkoani Mbeya.
Alisema fedha alizopata zitamsaidia kuongeza mtaji wa biashara yake ambayo imekuwa ikisuasua kutokana na mtaji mdogo huku fedha zingine akizielekeza kulipia karo za watoto wanaosoma shule binafsi.
Iddi Yusuph (26) mkazi wa Iringa alisema ni vema Watanzania na wateja wa Airtel wakaamini kuwa kichezo hiyo ipo na inafanyika kweli wala sio utapeli na haifanyiki kwa kujuana na watumishi wa airtel kwani yeye mwenyewe ameshinda pasipo kutoa chochote wala kujuana na mtumishi yeyote.
Baadhi ya mashuhuda wa mashindano hayo walisema ni jambo zuri linalofanywa na Kampuni ya Airtel kwa kuweka mashindano ya wazi ambapo kila mtu anaona namna mshiriki anavyohangaika kuokjota fedha kutoka kwenye boksi na kwamba hali hilyo huonesha kuwa hakuna upendeleo.