Historia
Asili ya jina Mbeya ni neno la Kisafwa ‘Ibheya’
likimaanisha chumvi. Wafanyabiashara wengi walifika eneo hilo
kubadilisha chumvi na mazao yao. Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na
wakoloni Waingereza mwaka 1927 kufuatia kushamiri kwa upatikanaji wa
dhahabu kwenye milima ya Loleza na mkondo wake kufika Chunya eneo la
Lupa Tingatinga. Hata leo eneo la kati la jiji la Mbeya huitwa Lupa Way
kama ilivyozoeleka miaka hiyo ambapo mahema ya wafanyabiashara wa
Kihindi yaliwekwa wakiwa njiani kwenda Lupa.
Jografia ya mji wa Mbeya na historia ya makanisa makongwe iliathiriwa na ubaguzi uliowekwa na wakoloni Waingereza.
Eneo la Uzunguni lilitengwa kwa ajili ya Waingereza waliokuwa watawala.
Hata makao makuu ya serikali ya Jimbo yalikuwa eneo hilo. Hivyo kanisa
la Waingereza, Anglikana limejengwa mwanzo wa Uzunguni karibu kabisa na
makao makuu ya mkoa na wilaya ya Mbeya.
Eneo la Uhindini, Lupa
Way litengwa kwa ajili ya Wahindi kutoa Goa walikuwa wakifanya biashara
hapo. Kwa kuwa kanisa la Katoliki lilikuwa likihudumia Wahindi hao na
wazungu wachache Waeire (Irish) lilijengwa katikati la eneo la Uzunguni
na Uhindini.
Eneo la Majengo litengwa kwa ajili ya Waafrika.
Kanisa la Moravian ambalo ndilo dhehebu la Kikristo asilia la Mbeya,
lilijengwa Majengo karibu na Sokomatola ambako Waafrika waliishi.
Miongoni mwa Waingereza hapakuwepo na Mmoravian hata mmoja.
Mji
wa Mbeya uliendelea kupanuka pande zote isipokuwa eneo la Kaskazini
lilitawaliwa na milima. Ujio wa Wanyakyusa kutoka Rungwe ndiyo ulioleta
Uluteri mjini Mbeya.
Wakazi
Wasafwa ambao ndiyo wenyeji
halisi wa mji wa Mbeya wamekuwa wakihamia milimani kupisha wageni. Kukua
kwa kasi kwa jiji la Mbeya kumepelekea wenyeji hao kuuza maeneo yao na
wao kurudi maeneo ya milimani wakiendelea na kilimo na ufugaji kidogo.
Leo hii eneo la wilaya ya Mbeya ambako ndipo jiji lilipo limetawaliwa
zaidi na Wanyakyusa na Wakinga wakiwa ndiyo wafanyabiashara wakubwa na
Wahindi pia.
Wenyeji wengine wa wilaya ya Mbeya ni Wamalila.
Wenyeji wa wilaya za Rungwe na Kyela ni Wanyakyusa. Wenyeji wa wilaya
ya Ileje ni Wandali. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu ingawa watu
waishio huko zaidi ni Wanyiha. Wenyeji wa wilaya ya Mbozi ni Wanyiha na
Wanyamwanga, lakini mji wa Tunduma umetawaliwa zaidi na Wakinga ambao
ndiyo wafanyabiashara wenye kumiliki uchumu wa mji huo mdogo. Wenyeji wa
wilaya ya Mbarali ni Wasangu, Wawanji, Wabena na Wakinga.
HII NI MBEYA WANAKOPATIKANA WANYAKYUSA
No comments:
Post a Comment