Sunday, January 31, 2016

Mkuu wa Shule ya Sekondari Komakya avuliwa madaraka.



kili

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Novatus Makunga amelazimika kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komakya iliyoko Mkoani Kilimanjaro kufuatia kukiuka maagizo ya Mkuu wa Mkoa ya kuwa vikao vyote vinavyohusiana na michango ya wanafunzi kati ya wazazi na uongozi  wa shule kutolewa ufafanuzi kabla michango hiyo haijaanza kukusanywa
Hatua hiyo imekuja kufuatia simtofahamu iliyojitokeza kati ya wazazi wa wanafunzi na uongozi wa shule uliotolewa ya kwamba kabla ya michango kukusanywa ni lazima Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupewa Taarifa.
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Komakya iko umbali wa km 18 kutoka moshi mjini amelalama kuhusu kupoteza muda mwingi akifuatilia ada.
Sintofahamu ilijitokeza   kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo mara baada tu walimu wa shule iyo kuwarudisha ada wanafunzi huku wakitaka kupewa ufafanuzi kuhusiana tamko la mh. Rais kuhusu elimu bure
Kufuatia suala hilo Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini Novatus Makunga akalazimika kufika shuleni hapo na baada ya kusikiliza pande zote kumvua madaraka Mkuu wa Shule hiyo Bi.Rose Ngoti kufuatia kufanya maamuzi na wazazi wa shule kwa kuchangisha michango pasipo kuishirikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama waraka wa seriklai unavyozitaka shule hizo
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mjini ina jumla ya shule za Kata 57 wanafunzi 25,402 walimu 1300 huku changamoto kubwa ikiwa ni upungufu wa walimu wa sayansi katika shule hizo.

Zoezi la kutoa kivuko kilichozama lakutana na wakati mgumu

kivuko

Licha ya kuwasili kwa mitambo  kusaidia zoezi la uokoaji wa kivuko kilichozama, zoezi hilo limeshindwa kufanyika kwa ufanisi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha toka saa saba usiku hadi majira ya saa kumi jioni kukwamisha zoezi hilo pamoja na juhudi za kuvuta kivuko hicho kushindikana.
Hata hivyo huduma ya mawasilinao baina ya upande wa Ulanga na Kilombero imeweza kurejea mara baada ya Wizara ya mawasilinao ujenzi na uchukuzi kufanikiwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu ili waendelee na safari.
Zoezi la uokoaji na uvutaji wa kivuko  ch MV Kilombero limezidi kuwa gumu, kutokana na changamoto ya vifaa vya uokozi, pamoja na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo  hilo, hivyo kukwamisha juhudi zinazoendelea kutolewa na mamlaka za uokozi.
Licha ya kutumia helkopta ya jeshi la Polisi kutafuta kama kuna watu ambao walisombwa na maji, juhudi hizo zimegonga mwamba baada ya kutopatikana kwa mtu hata mmoja.
 Hata hivyo juhudi zilizofanywa na wizara ya uchukuzi kwa kushirikiana na vikosi vya uokoaji kutoka kikosi cha wanamaji, vimefanikiwa kurudisha mawasiliano ya pande hizo mbili, kwa kuanza kuvusha wananchi wa kilombero na ulanga kwa kutumia boti za mwendo kasi. .
Wananchi wameiomba serikali kuongeza jitihada katika zoezi la uokoaji, na kuishukuru kwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu.
Zoezi la kukitoa kivuko na kukivuta nchi kavu  limeshindikana kwa siku ya jana kutokana  na kunyesha kwa mvua hiyo pamoja na mitambo iliyopelekwa kuvuta, kushindwa kufanikiwa.

Wahitimu vyuo vikuu kupatiwa ujuzi .


Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo ya fani wanazosomea na badala yake watumie fursa zilizopo kujiongezea ujuzi wa kufanya kazi.
Rai hiyo imetolewa kufuatia wasomi wengi kudaiwa kushindwa kuajiriwa kwa kukosa ujuzi wa fani walizosomea.
 Ni katika mkutano wa wajasiriamali na wakufunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ,  ambapo Prof Ganka Nyamsoro, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Tawi la Dar Es Salaam amesema,  chuo hicho kimechaguliwa kusimamia mradi wa kuwasaidia wahitimu kupata nafasi katika kampuni  za wajasiriamali ili waweze kujiongezea uzoefu  na kupata ajira.
Mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la SWEDENI umelenga kutoa fursa kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu kupata uzoefu wa yale waliyosomea chuoni.
 Kwa upande wa Wajasiriamali hao  wadogo na kati wamesema kwao ni Fursa Muhimu Kwakuwa watafanya kazi na watu wenye Taaluma,Huku wahitimu nao wakipata  ujuzi kutoka kwao.
Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la ajira mbali na kuwa Serikali imejitahidi kuwekeza katika elimu.

Hii Ndio Sababu ya Rais Magufuli Kumuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange..

RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .

Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Friday, January 29, 2016

TUNDUMA AND NAKONDE ENVIRONMENT.

UJASILIAMALI NA BIASHARA .

     
  Pata mambo matamu ili kama ni mwajiriwa au umeajiliwa soma HAPA MAUJANJA UJASIRIAMALI NA BIASHARA KIUJUMLA.
Nimekuwa nikishauri watu wanaoingia kwenye biashara na ujasiriamali kwa muda sasa lakini sijawahi kumwambia mtu aache kazi haraka ili aweze kuweka nguvu zake kwenye ujasiriamali. Nina sababu nyingi kwa nini sifanyi hivyo, na hapa nitakushirikisha sababu kumi.

1. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato cha uhakika. Japokuwa kazi haina uhakika sana kwa sasa, lakini angalau kwa sasa kuna kipato ambacho unakipata kwenye ajira yako. Hiki kitakuvusha nyakazi ambazo ni ngumu, hasa pale ambapo utaanza ujasiriamali ukiwa bado kwenye ajira yako.

2. Kuna nafasi nyingi za kuweza kuanza ujasiriamali hata bado ukiwa kwenye ajira yako. Tumia nafasi hizi na anza kidogo kidogo, jifunze kwenye kila hatua unayoshindwa au kukosea, endelea kukuza biashara yako na ikifikia hatua ukaona sasa hapa inaweza kukupatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yako ndio unaweza kuacha kazi.

3. Kutoa fedha kwenye biashara changa ni kuiua. Katika miezi angalau sita ya kwanza ya biashara yoyote ndio kipindi ambacho biashara yoyote inakazana kukua. Sasa kama utaondoa fedha kwenye biashara hii kwa sababu yoyote ile, unakuwa umeandika adhabu ya kifo kwneye biashara yako. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato kingine unachotegemea tofauti na biashara hiyo, hivyo kama umeajiriwa, hiki ndio kipato chenyewe.

4. Kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unapokuwa kwneye kazi ni rahisi sana kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unaweza kutengeneza wateja wengi wa huduma au bidhaa zako kupitia kazi unayofanya hivyo inakupa nafasi nzuri ya kuweza kukuza biashara yako.

5. Kufaidi huduma nyingine muhimu. Kuna huduma muhimu ambazo utaweza kuzifaidi kama utakuwa kwenye kazi. Kupitia kazi yako unaweza kuwa unapata huduma ya bima ya afya kwako na kwa familia yako. Hii inakusaidia kuokoa fedha nyingi ambazo ungezitumia kwenye huduma za afya. Japokuwa unaweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya kama mtu binafsi, bado itakugharimu kiasi kikubwa kuliko aliyeko kwneye ajira.

6. Kazi inaweza kukupa uzoefu wa biashara. Kuna baadhi ya biashara unazoweza kuanzisha ambazo zinaendana na kazi unayofanya sasa. Kwa kuwepo ndani ya kazi ile unajifunza mambo yote muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kukuza biashara yako. Pia unawajua vizuri wateja ambao wanaweza kuja kuwa wateja wako pia na mambo mengine ya ndani ambayo yatakuwezesha kuendesha biashara yako vizuri.

MAMBO YA BOARDER KILA MTU YU BUZZ

http://lusakavoice.com/wp-content/uploads/2014/05/Nakonde-border.jpg